Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amelazwa hospitali

Rais wa zamani wa Afrika kusini, Jacob Zuma. July 19, 2021.

Idara ya  magereza imethibitisha kwamba Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma leo Agost 6 mwaka 2021 amelazwa kwenye hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya. Zuma mwenye umri wa miaka 79 amepangiwa kuhudhuria kuanza tena kwa kesi ya muda mrefu ya ufisadi hapo Agosti 10

Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma, aliyefungwa kwa kuidharau mahakama mwezi uliopita amelazwa hospitali leo Ijumaa chini ya wiki moja kabla ya kufikishwa mahakamani kwa kesi tofauti ya ufisadi.

Idara ya magereza imethibitisha kwamba Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma leo Agost 6 mwaka 2021 amelazwa kwenye hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya, ilisema taarifa hiyo. Zuma mwenye umri wa miaka 79 amepangiwa kuhudhuria kuanza tena kwa kesi ya muda mrefu ya ufisadi hapo Agosti 10.

Usikilizaji wa kesi hiyo utajumuisha ombi la kufutiwa mashtaka 16 ya ubadhirifu, rushwa na ulaghai dhidi yake katika kuhusika na ununuzi wa ndege za kivita mwaka 1999, boti za doria na vifaa kutoka kwa kampuni tano za silaha za ulaya wakati alipokuwa naibu wa rais.

Jacob Zuma, Rais wa zamani wa Afrika kusini

Zuma anashutumiwa kuchukua hongo kutoka kwa moja ya makampuni hiyo, kampuni kubwa ya ulinzi ya Ufaransa ya Thales ambayo imeshtakiwa kwa ufisadi na biashara haramu ya fedha. Kesi zimekuwa zikiahirishwa mara kwa mara kwa zaidi ya muongo mmoja na kuchochea shutuma ya mbinu za kuchelewesha kesi.