Wachambuzi, wanaharakati na waandishi habari katika kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wanasema matumaini makubwa yaliyokuwepo kutokana na mapinduzi yaliyongozwa na vijana kuanzia Tunisia, kupitia Misri kuelekea Libya, Yemen na hatimae Syria, ya kupigania mageuzi ya kijamii, uhuru wa kisiasa na kujieleza yalitoweka muda mfupi tu baada ya kuanza.
Kilichopatikana miaka 10 baada ya mapinduzi ya nchi za Kiarabu
Your browser doesn’t support HTML5
Mapinduzi ya nchi za kiarabu yaliyofahamika kama 'Arab Spring' yaliyowaondowa madarakani viongozi wa kimabavu wa nchi za kiarabu kuanzia Zine El-Abidine Ben Ali wa Tunisia, Hosni Mubarak wa Misri hadi Ali Saleh wa Yemen.