Mahakama ya Iran imefunga ofisi mbili za taasisi hiyo, ikizitaja kama vituo haramu vyenye uhusiano na serikali ya Ujerumani, ambayo imekiuka sheria za Iran, na kufanya vitendo vingi haramu na ukiukwaji mkubwa wa kifedha.
Mahakama imesema uchunguzi wa ziada katika vituo vingine vya Ujerumani unaendelea kwa sababu ya ripoti za ukiukwaji. Balozi wa Iran nchini Ujerumani amesema kufungwa kwa vituo vya dini ya Kiislamu ni chuki dhidi ya Uislamu na hatua ya uhasama.
Vituo hivyo vilifungwa mwezi Julai, vikishutumiwa kukuza na kueneza itikadi za kuunga mkono kundi la wanamgambo wa Hezbollah.
Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imesema imevipiga marufuku vituo hivyo kwa sababu taasisi za msimamo mkali zinatumia kupinga sheria za Ujerumani ambapo vituo 53 vilivamiwa.