Guterres ataka ukaguzi katika kinu cha nyuklia cha Ukraine

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa mwito wa kuruhusu wakaguzi wa jumuiya ya kimataifa katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzya baada ya Ukraine na Russia kulaumiana kutokana na kushambuliwa kwa kinu hicho hivi karibuni.

Kufanywa shambulizi lolote katika kinu hicho ni jambo la mauaji, Guterres aliwaeleza wanahabari katika mkutano.

Ukraine iliishutumu Russia kwa mara nyingine kwa shambulizi la Jumapili katika kituo kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, na kuishutumu Moscow inajiingiza katika ugaidi wa nyuklia.

Kampuni ya taifa ya nyuklia ya Ukraine imesema vikosi vya Russia viliharibu sensa tatu za mionzi katika shambulizi la Jumamosi usiku, na kujeruhi wafanyakazi waliokuwepo.