Serikali ya Finland imesema itafungua tena mipaka yake miwili kati ya nane inayokatisha katika mpaka wake wa kilomita 1,340 na Russia. Awali serikali ilikuwa imefunga mipaka yote minane kufuatia wimbi la ghafla la wahamiaji wanaoingia nchini humo kupitia Russia.
Finland iliripoti kuwa ilipokea takribani wahamiaji 1,000 kutoka Agosti hadi mwishoni mwa Novemba wakati nchi hiyo ilipofunga mpaka wake, huku wahamiaji 900 wakiwasili mwezi Novemba pekee, ongezeko kutoka kwa wahamiaji wachache, zaidi ya mmoja wanaowasili kwa siku.
Bila kuvunja masharti, hatuwezi kuthibitisha iwapo mabadiliko kwa ajili ya ubora yanafanyika. Kama hali itaendelea, tutafunga vituo hivi vya kukatisha mpaka, Waziri Mkuu Petteri Orpo alisema Jumanne katika mkutano na waandishi wa habari.
Wahamiaji hao waliwasili bila visa au nyaraka halali, wakitokea nchi kama vile Kenya, Morocco, Pakistan, Somalia, Syria na Yemen.