Uhamiaji, mabadililo ya hali ya hewa, biashara na viwanda ni baadhi ya masuala yanayotarajiwa kutawala ajenda ya kikao hicho. Biden aliwasili Mexico Jumapili jioni baada ya kuutembelea mji wa mpakani wa El Paso katika jimbo la Texas, ili kujionea mwenyewe maelfu ya wahamiaji wasio na stakabadhi, wanaojaribu kuingia Marekani wakitokea Mexico.
Biden aliyechukua takriban saa nne kwenye mpaka huo alifuatana na maafisa wa mpakani huku akijionea namna wanavyokagua magari wakitafuta dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa fedha, pamoja na bidhaa nyingine kinyume cha sheria.
Biden pia aliandamana na maafisa hao kwenye uzio unaotenganisha Marekani na Mexico. Pia alitembelea kituo cha uhamiaji cha El Paso ambako alikutana na maafisa wa uhamaji pamoja na viongozi wa kijamii.
Baada ya kuutembelea mpaka huo, Biden aliweka ujumbe kwenye Twitter akiesema kwamba inawezekana kuulinda mpaka wa Marekani na Mexico na kuufanya mpaka huo kuwa salama kwa wahamiaji.