Wachambuzi Afrika watoa maoni yao

Hotuba ya Hali ya Taifa aliyotoa rais wa Marekani Barack Obama Jumatano, ilitizamwa kote duniani na hata katika bara la Afrika ambapo wengi wanamwona rais huyo kuwa mmoja wao.

Akizungumza na sauti ya Amerika Prof. Xavery Lwaitama wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam Tanzania, alisema rais Obama anaonekana kupoteza shauku aliyokuwa nayo alipogombania urais. Alisema hili huenda limetokana na changamoto anazokabiliana nazo za kurithi uchumi uliodorora, na kupotea kwa ajira.

Hata hivyo Prof. Lwaitama anasema hotuba ya bwana Obama inapaswa kuwa somo kwa viongozi wa Afrika, kueleza ukweli, wa hali halisi ya mataifa yao na kushauriana na wenzao hata ikiwa wako upande wa upinzani kwa maslahi ya nchi zao.