Majengo ya Uingereza lazima yawe na vyanzo vya umeme wa magari

Uingereza Jumapili imetangaza kwamba majengo mapya yatapaswa kuwa na sehemu za kuchajia magari ya umeme kuanzia mwaka ujao.

Kwa mujibu wa sheria mpya ambayo itatangazwa na waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, inaeleza kuwa majengo mapya yatahitajika kufuata kanuni hiyo kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya waziri mkuu.

Inaeleza kwamba kanuni hizo zitafanikisha kuwepo na sehemu za kuchajia magari 145,000 zaidi ambazo zitafungwa Uingereza kila mwaka mpaka itakapifikia mwaka 2030 wakati ambapo mauzo ya magari yanayotumia mafuta ya Petroli ama Diesel yatasitishwa.

Kanuni hizo pia zitahitajika kwa nyumba mpya na majengo yasiyo makazi ya watu kama vile maofisi na maduka makubwa ya mahitaji.

Pia itajumuisha majengo yanayofanyiwa ukarabati mkubwa ambayo yatahitajika kuwa na sehemu za maegesho ya magari mpaka 10.