Hilo ni tukio la pili la aina hiyo ndani ya wiki mbili, wakati Pyongyang ikiendelea kuimarisha ulinzi wake kwenye mipaka yake na Kusini. Milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini karibu na mpaka huo pia imejeruhi wanajeshi kadhaa wa Korea Kaskazini, mkuu wa majeshi wa Kusini amesema, akiongezea kuwa Pyongyang hivi karibuni ilituma wanajeshi wake kwenye eneo hilo ili kufanya usafi, na kuweka mabomu ya ardhini, wakati uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ukiendelea kudorora.
Mataifa hayo yamebaki katika hali ya vita baada ya mgogoro wa 1950- 1953 kumalizika, na kila mmoja kubaki akiwa amejihami, wakati eneo la mpaka lisilo na jeshi linaloigawa peninsula hiyo likisemekana kuwa na mabomu mengi ya kutegwa ardhini hapa duniani. Lakini Korea Kaskazini imeendelea kuimarisha uwekaji mabomu ya kutegwa ardhini, na kuimarisha mbinu za barabara na kuongezea kile ambacho kinaonekana kuwa vizuizi dhidi ya vifaru, jeshi la Seoul limesema.
Forum