Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:22

'Wasikilize watu wa upande wa huku,' Wahamiaji wa Mexico wanasema wakati Biden akifanya ziara mpakani


Julio Marquez na Yalimar Chirinos, wahamiaji kutoka Venezuela.
Julio Marquez na Yalimar Chirinos, wahamiaji kutoka Venezuela.

Mhamiaji  kutoka Venezuela  Julio Marquez, muuza  peremende  karibu na eneo la mpakani kaskazini mwa  mji wa Ciudad Juarez, ulioko Mexico amebeba  bango  lenye maandishi yanayosomeka: “ Tusaidie  kwa chochote kinachotoka moyoni mwako.” 

Ana ujumbe kama huo kwa rais wa Marekani Joe Biden aliyefanya ziara katika jimbo la Texas kwenye mji wa mpakani wa El Paso, siku ya Jumapili.

“Tuna matumaini atatusaidia, atatuachi tupite , kwa vile tunateseka sana hapa Mexico” amesema Marquez mwenye umri wa miaka 32. “ Lazima awasikilize watu wa upande huu.”

Hii ni ziara ya kwanza ya rais Biden ambayo imefanyika siku kadhaa baada ya kupitishwa sera mpya inayolenga kupunguza haramu ambayo imekosolewa na watetezi wa uhamiaji kuwa inaweka vizuizi kwa wale wanaoomba hifadhi .

Mwelekeo wa njia mbili zinazotumika zinatoa mamlaka ya kisheria kwa baadhi ya raia wa Cuba, Nicaragua, Haiti na Venezuela wenye wadhamini nchini Marekani, wakati ikiruhurusu kuwarudisha watu wa mataifa hayo kurejea Mexico iwapo watajaribu kuvuka mpaka bila kibali.

Afisa wa uhamiaji wa Mexico na polisi siku ya Jumamosi walifanya doria katika kingo za mto Rio Grande unaotenganisha mji wa Ciudad Juarez and El Paso, wakati makundi ya familia zikijaribu kuruka senyenge na kuingia Marekani.

Marquez amesema yeye na mwenzake Yalimar Chirinos, mwenye umri wa miaka 19, hawana vigezo vya kuingia Marekani kulingana na sheria mpya kwa kuwa hawana mfadhili nchini Marekani.

“ Wanabadilisha sheria kila wakati, kila wiki”, Chirinos amesema, akiwa amevaa fulana nyeusi ‘hoodie’ na glovu moja ya pink na nyingine ya bluu akijihifadhi na baridi.

Wawili hao wameishi Mexico kwa miezi mitano baada ya kuvuka mipaka ya nchi kadhaa ukiwemo msitu hatari wa Darien ulipopo kati ya Colombia na Panama. Wakilala nje bila kuwa na turubai wala blanketi, wakijipa joto kwa kukumbatiana, wakihofia wahalifu wanaojulikana kupora na kuwateka wahamiaji.

Chanzo cha habari hizi ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG