Kufikia mwezi Oktoba 2022, Tanzania ilikuwa inadaiwa shilingi trilioni 64 ikiwa ni deni ambalo nchi hiyo inadaiwa na nchi au wafadhili wan je, ambayo ni asilimia 70.6 ya deni la jumla la serikali.
Wakopeshaji wa ndani wanadai serikali shilingi trilioni 26.6.
Sekta ya uchukuzi na mawasiliano inaongoza kwa kiasi kikubwa cha deni, zikifatiwa na huduma kwa jamii, elimu, nshati na madini.
Wakopeshaji wakuu wa ndani ya nchi ni kutoka kwa mfuko wa pensheni pamoja na benki za biashara, ikiwa inafikia kiwango cha asilimia 55.8 cha deni la jumla la serikali.
Kulingana na gazeti la The Citizen, waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchema, alisema mwezi Juni mwaka huu kwamba ongezeko la deni la serikali linatokana na kuongezeka kwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Serikali ya Tanzania imesema kwamba japo deni la linaendelea kuongezeka, ina uwezo wa kulipa.