Hivi sasa linafanya safari zake katika soko lililofurika biashara ya usafiri wa ndege barani Afrika, ambapo mashirika ya ndege yanasuasua kifedha na ndege zao hazina abiria kuliko ndege zote maeneo mengine ulimwenguni.
Shirika hilo la ndege la serikali lilianzisha ndege za abiria Jumatano, kwa mara ya kwanza tangu lilipofilisika mwaka 2001. Linalo lengo la kuchukuwa sehemu ya soko la biashara ya usafiri wa anga ambayo hivi sasa inahodhiwa na shirika la ndege la Ethiopia, shirika ambalo linajulikana kwa mafanikio yake.
Nchi zilizowekeza katika mashirika yao
Shirika la habari la Reuters linaripoti pia Uganda ni serikali ya Afrika ambayo hivi karibuni imewekeza fedha ikiwa kati ya serikali za Afrika zilizofanya hivyo katika mashirika yao ya ndege ya taifa ; Tanzania na Senegal pia zimefufua mashirika yao ya ndege, wakati Rwanda, Ivory Coast na Togo wanayaongezea uwezo mashirika yao.
Lakini juhudi kama hizi zimekutana na vipingamizi vingi vinavyotokana na kuongezeka gharama za uendeshaji wa biashara hiyo na pia kuyalinda masoko yao, jambo ambalo limezuia utekelezaji wa mkataba wa anga huru wa mabara ulimwenguni – kitu ambacho wachambuzi katika sekta hiyo wanasema ni muhimu kwa mafanikio ya mashirika ya ndege ya Kiafrika katika masoko yenye ushindani mkubwa.
Makadirio ya ukuwaji wa soko la Afrika
Soko la Afrika linatabiriwa kuwa litakua angalau kufikia asilimia 5 kwa mwaka kwa kipindi cha miongo miwili ijayo kwa ubebaji abiria, kwa haraka zaidi kuliko masoko yaliyokomaa kiutendaji, kulingana na Jumuiya ya Usafiri wa Anga wa Kimataifa (IATA).
Hata hivyo, hiki ni kiwango cha chini na mashirka mengi ya ndege yanayomilikiwa na serikali katika eneo yanaendelea kupoteza fedha.
Wakati sekta ya usafiri wa anga duniani ikiwa vizuri katika kuingiza faida ya dola za Marekani bilioni 28, mashirika ya ndege ya Afrika yanakadiriwa kuwa yatapoteza kwa pamoja dola milioni 100 mwaka huu, IATA imesema mwezi Juni, 2019.
Mkakati wa Uganda
Shirika la ndege la Uganda, kama ilivyo kwa washindani wake kibiashara, inalengo la kuvutia wasafiri wa ndani ya nchi kuweza kujikwamua kutokana na hali mbaya inayoendelea kibiashara katika bara la Afrika. Takriban wasafiri milioni 2 kila mwaka wanasafiri kupitia Entebbe, uwanja wa ndege mkuu, Uganda. Kiasi cha abiria asilimia 70 ni wananchi wa Uganda, amesema mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Ephraim Bagenda.
“Wale wote hivi sasa wanaosafiri na ndege ya mashirika ya nje,” ameliambia shirika la habari la Reuters, “Tunataka sehemu ya keki hiyo.”
Mkataba wa anga huru
Mwaka 2018, ilionekana kama Afrika ilikuwa inapiga hatua katika mkataba wa anga huru – Soko la pamoja la Usafiri wa Anga la Afrika – ili kuyawezesha mashirika ya ndege kuamua kwa kiasi gani wanaweza kupeleka ndege zao kati ya miji mbalimbali na aina ya ndege wanaweza kutumia.
Jumla ya nchi 28 wamesaini mkataba huo, wakiingia katika hisabu inayofanya asilimia kati ya 75-80 ya usafiri wa anga wa Afrika. Uganda inafikiria kusaini mkataba huo, Waziri wa Ujenzi na Usafiri Monica Azuba Ntege amesema.
Hata hivyo, mpaka sasa waliosaini mkataba huo – ni pamoja na Cape Verde, Ghana, Togo, Ethiopia na Nigeria – wameanza kubadilisha sheria zao kutekeleza makubaliano hayo na kufunga masoko yake, amesema Raphael Kuuchi, Makamu wa Rais katika bara la Afrika katika IATA.