Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 01:09

Modi ametabiriwa kupata ushindi mkubwa India


Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia katika mojawapo ya shughuli za kuzindua miradi ya maendeleo
Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia katika mojawapo ya shughuli za kuzindua miradi ya maendeleo

Chama tawala nchini India cha Bharatiya Janata BJP, cha Waziri Mkuu Narendra Modi kimetabiriwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliomalizika Jumamosi.

Ukusanyaji wa maoni baada ya upigaji kura unaonyesha kwamba chama hicho kitafanya vyema ikilinganishwa na maoni ya wachambuzi kadhaa wa siasa za nchi hiyo.

Ukusanyaji maoni unaonyesha kwamba muungano unaotawala wa National Democratic Alliance NDA, huenda ukapata theluthi mbili ya viti katika bunge lenye viti 543.

Mshindi kwenye bunge anahitaji viti 272 kuwa na wingi mdogo na theluthi mbili ya viti itatoa fursa kwa serikali kutekeleza marekebisho makubwa kwenye katiba ya nchi.

Ukusanyaji maoni baada ya uchaguzi, na mashirika tofauti unaonyesha kwamba muungano wa NDA huenda ukapata kati ya viti 353 na 401. Chama cha BJP huenda kikapata viti 303

Muungano wa upinzani wa India Alliance, unaoongozwa na chama cha Congress, cha Rahul Ghandi, kimetabiriwa kupata kati ya viti 125 na 182.

Forum

XS
SM
MD
LG