Ndege ya abiria ya Libya imeanguka katika mji mkuu Tripoli na kuuwa kila mtu ndani ya ndege hiyo isipokuwa mtoto mmoja wa kiholanzi.
Maafisa wa usalama wa Libya wamesema ndege ya shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa inatokea Johanesburg Afrika Kusini Jumatano asubuhi ilipoanguka hatua chache kabla ya kufika kwenye njia yake kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.
Waziri wa usafirishaji wa Libya Mohamed Ali Zidan amesema wachunguzi wanajaribu kuchunguza nini kimesababisha ajali hiyo. Aliondoa uwezekano wa ugaidi.
Kulikuwa na abiria 93 na wafanyakazi 11 kwenye ndege hiyo aina ya Airbus A330.
Maafisa wa utalii wa Uholanzi wanasema 61 kati ya waliouwawa walikuwa ni raia wa Uholanzi.