Kiongozi wa wanaopigana na serikali ya Ethiopia anasema wanajeshi wake wako karibu na mji mkuu na wanatayarisha shambulizi jingine, akitabiri kwamba vita vitaisha hivi karibuni huku wanadiplomasia wakiharakisha kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano.
Jaal Marroo, kamanda wa jeshi la Oromo Liberation Army(OLA) alimuonya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwamba wapiganaji wanaoiunga mkono serikali wanajiengua na kwamba wapiganaji wao walikaribia kupata ushindi. Jaal ambaye jina lake halisi ni Kumsa Diriba, aliliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano jana Jumapili.
Alisema kuwa kile ambacho ana uhakika nacho ni kwamba vita vitakwisha hivi karibuni akiongeza kuwa wanajiandaa kushinikiza uzinduzi mwingine na shambulizi jingine. Serikali inajaribu tu kuvuta muda na wanajaribu kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo hivyo wanatoa wito kwa taifa kupigana.