Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 01:32

Biden na Zelenskyy kukutana Italia


Rais Joe Biden, wa Marekani, na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, wanatazamiwa kutia saini makubaliano ya muda mrefu ya ulinzi na usalama Alhamisi katika mkutano wa nchi saba tajiri nchini Italia.

Kutia saini makubaliano hayo, amesema mshauri wa usalama wa kitaifa wa White House Jake Sullivan, kunatoa taarifa kwa Russia, kuhusu azimio la Marekani.

“Ikiwa Rais wa Russia, Vladimir Putin, anafikiri anaweza kuushinda muungano unaounga mkono Ukraine, amekosea,” amesema Sullivan, ambaye aliongeza kuwa makubaliano hayo ambayo tayari yametiwa saini na nchi nyingine 15, hayatapeleka wanajeshi wa Marekani moja kwa moja katika ulinzi wa Ukraine, dhidi ya uvamizi wa Russia.

“Tutaendelea kuongeza gharama katika vita ya Russia,” msemaji wa White House, John Kirby aliwaambia wanahabari Jumanne. “Tutatangaza hatua mpya za kuthaminisha mali za Russia, ili kuifaidisha Ukraine katika ahueni kutokana na uharibifu ambao jeshi la Putin limesababisha.”

Forum

XS
SM
MD
LG