Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 01:42

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kujadili hali ya Rafah


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa wanahabari wakati wa mkutano wa BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Alhamisi, Agosti 24, 2023.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa wanahabari wakati wa mkutano wa BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Alhamisi, Agosti 24, 2023.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kukutana Jumanne kujadili hali ya Rafah kufuatia shambulizi la anga la Israel lililoua Wapalestina 45 waliokuwa wakijihifadhi katika kambi ya wakimbizi na kuwajeruhi wengine 200.

Kabla ya mkutano huo, wafanyakazi wa matibabu na wakazi waliripoti mashambulizi mapya ya anga ya Israeli Jumanne katika eneo la kambi hiyo vikosi vya Israeli vilipiga Jumapili.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina lilisema Jumanne kwamba zaidi ya watu milioni 1 wamekimbia Rafah katika kipindi cha wiki tatu zilizopita huku Israel ikishambulia.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths alitoa taarifa Jumatatu usiku akiita shambulio la Jumapili "halikubaliki kabisa" na kukosoa maelezo ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba kilichotokea Rafah ni "kosa la kusikitisha."

Forum

XS
SM
MD
LG