Vikosi vya Marekani vilivyopewa jukumu la kukabiliana na kundi la kigaidi la al-Shabab havitalazimika tena kusafiri hadi Somalia kutoka nchi jirani baada ya maafisa kutengua uamuzi ambao maafisa wanalaumu kwa kuruhusu ushirika wa al-Qaida kukua na kuwa na nguvu zaidi na hatari sana.
Hapo Jumatatu Rais Biden aliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi wasiozidi 500 katika taifa hilo la Afrika mashariki ili kuwa na idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani nchini Somalia katika juhudi za kulilenga vyema kundi la al-Shabaab na viongozi wake afisa mwandamizi wa utawala aliwaambia waandishi wa habari.
Uidhinishaji huo mpya unabatilisha uamuzi wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wa Disemba mwaka 2020 wa kuwaondoa wanajeshi 700 wa kikosi maalum ambao walikuwa wametumwa Somalia kufanya kazi na wanajeshi wa Somalia na kuwataka badala yake waingie nchini humo mara kwa mara kusaidia hatua ambayo utawala wa sasa ulikataa na kusema kwamba ni mbaya.
Tangu wakati huo al-Shabab kwa bahati mbaya imekuwa na nguvu zaidi afisa wa White House alisema akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina ili aweze kuzungumzia uidhinishaji huo mpya.